Hotuba Ya Mwenyekiti Wa Bodi Ya Tpsf, Bi. Angelina Ngalula Katika Kongamano Kuu La Biashara Nchini Pamoja Na Mkutano Mkuu Wa Ishirini Na Moja Wa Wanachama Wa Tpsf (21st AGM) Wa Mwaka Tarehe 11th December 2021, Maktaba Mpya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.

Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa:Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Godfrey Mwambe: Waziri wa Uwekezaji
Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo: Waziri wa Viwanda na Biashara
Mheshimiwa Dr. Damas Ndumbaro: Waziri wa Utalii na Maliasili
Mheshimiwa Lela M. Mussa-Waziri wa Utalii na maliasili-Zanzibar
Mheshimiwa John Mongela: Mkuu wa Mkoa wa Arusha na mwenyekiti wa wakuu wa mikoa
Mheshimiwa Martin Shigella: Mkuu wa mkoa wa Morogoro
Mheshimiwa Zainabu Telaki: Mkuu wa mkoa wa Lindi
Waheshimiwa mabalozi mliopo hapa natambua uwepo wa Balozi Edwin Rutegaruki, Balozi wa Uturuki, Balozi wa Rwanda
Wahesimiwa Mawaziri Wastaafu: Natambua uwepo wa Mh. Charles Mwijage Waziri wa Viwanda na Biashara Mstaafu.
Makamu Mwenyekiti wa Tasisi ya Sekta Binafsi na Mwenyekiti wa CTI- Paul Makanza
Bodi ya Wakurugenzi wa Tasisi ya Sekta binafsi
Secretariet ya Tasisi ya Sekta binafsi
Dr. Godwill Wanga-Katibu Mtendaji wa baraza la Taifa la Biashara, natambua uwepo wa Dada yangu Bengi Issa mtendaji mkuu wa Baraza la uwezeshaji wa Taifa.
Viongozi wa Tasisi za serikali na Sekta binafsi wote mliopo hapa
Sponsors wote
Waandishi wa habari
wageni wote waalikwa
Mabibi na mabwana
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Mhe. Mgeni rasmi, awali ya yote, nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kujumuika pamoja kwa ajili ya mkutano wetu Mkuu wa 21.

Mhe. Mgeni rasmi,
Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi ya TPSF, Sekretarieti na wadau wa sekta binafsi Tanzania, napenda kutoa shukurani zetu za dhati;

Kwanza:Naomba nichukue nafsi hii kwa niaba ya Sekta Binafsi kutoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya 6 chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa jinsi alivyoboresha mashirikiano ya serikali na sekta binafsi na pia kwa kazi kubwa ambayo serikali ya awamu ya sita inavyoendelea kuifanya ya kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji wa nje na wa ndani pamoja na kuimarisha mahusiano na nchi mbalimbali.

Tayari matunda ya kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita ya kuboresha mazingira ya biashara na mahusiano imeanza kuzaa matunda. Katika kipindi kifupi kumekuwa na ongezeko la biashara na uwekezaji na nchi zote alizozitembela Mh. Rais wetu. Mfano kwa mara ya kwanza bidhaa za Tanzania zinazoingia nchini Kenya imezidi bidhaa za Kenya zinazoingizwa nchini Tanzania. Tumeshuhudia pia wawekezaji wakubwa kutoka nchi ya Burundi uwekezaji wa kiwanda kikubwa cha mbolea, Marekani wawekezaji wakubwa kwenye sekta ya nishati (Renewable energy) umeme wa upepo tayari kampuni kubwa ya Marekani ipo tayari kuwekeza Umeme wa upepo mkoani Singida, sekta ya utalii tayari Billionenaire mkubwa wa marekani ameonesha nia ya kuwekeza hotel ya nyota Saba mkoani Lindi.

Faida za uboreshaji wa mazingira situ zimeongeza wawekezaji wapya kutoka nje bali hata kampuni za ndani zimeanza kupanua shughuli za uzalishaji ukienda Geita utaona Dada yangu Sarah Masasi anavyoongeza uwekezaji kwenye kiwanda cha dhahabu, viwanda vya sukari Kilombero, Kagera na maeneo mengine mengi lakini pia wafanyabiashara ndogo ndogo wameanza sasa kufanya biashara katika mazingira mazuri Zaidi na mfano mzuri eneo la coco beach.

Pili –naomba upokee shukurani zetu wewe binafsi kwa kukubali kuwa mgeni Rasmi na kutenga muda wako kushiriki mkutano wa 21 wa Tasisi ya sekta binafsi wenye kauli mbiu “ Kuimalisha ushirikiano wa sekta ya Umma na Sekta binafsi kwamaendeleoendelevu” kuwa nasi siku ya leo tukitambua shughuli nyingi za kitaifa ulizonazo.

Hii ina maana kubwa kwetu kwani ni ishara ya kuwa serikali yetu iko tayari kushirikiana na sekta binafsi kama mshirika wake mkubwa katika kuchochea na kuimarisha maendeleo endelevu ya kiuchumi. Tunasema Asante Sana!

Tatu, Mh. Mgeni rasmi, napenda nichukue nafasi hii kuipongeza serikali ya JMT kwa kuhitimisha kilele cha sherehe za uhuru wa nchi yetu. vilevile, Tunampongeza Mh. Dkt. Hussein Mwinyi, Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa maandalizi ya jukwaa la uwekezaji, ambalo lililenga kutathimini mchango wa sekta binafsi katika uchumi na kuainisha, ama kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi.

Mh. Mgeni rasmi naomba uniruhusu kwa kifupi kuzungumzia MAFANIKIO YA MWAKA 2020/2021 ya TASISI ya SEKTA BINAFSI
Katika mwaka 2020/2021 TPSF imepata mafanikio makubwa kutokana na mpango kazi wetu na ushirikishwaji wa wadau wa Sekta binafsi kama ifuatavyo:

1.) Eneo la kwanza: Tumefanikiwa kuwa na Tasisi ya Sekta binafsi shirikishi ya makundi yote kuanzia wafanyabiashara ndogo ndogo, akina mama na vijana na hata wazee. Utaona hata hapa leo tuna uwakilishi wa wafanyabiashara wa aina zote kutoka sekta mbali mbali mikoani. Tuna umoja wa wachimba madini wanawake kutoka Mererani, Wanawake wachimba dhahabu kutoka Geita, Umoja wa Wanawake Wavuvi kutoka Bukoba, Umoja wa Wanawake wa kampuni za ujenzi (Contractors), Machinga na makundi mengine mengi

2.) Eneo la pili: Tumeweza kuwahamasisha wafanyabiashara wadogo wadogo kujiunga kwenye vikundi na ili waweze kushiriki kutoa huduma kwenye miradi mikubwa ya kimkakati. Kupitia Kongamano la Sekta binafsi tulilofanya Mwanza kwa kushirikiana na shirika la reli TRC tuliwahamasisha wafanyabishara kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata kazi na kuweza kukopesheka. Napenda kukujulisha hapa ndani ya Ukumbi tuna kikundi cha akina mama wajasiliamali kanda za ziwa kijulikanacho kamaUWWAKAZI ni moja ya kikundi kilichofanikiwa kupata kazi kubwa ya kutoa huduma ya chakula kwenye mradi wa SGR Lot.5 baada ya wajasiliamali hawa kuungana na kusajili kikundi chao. Kazi ya kuwahamasisha wafanyabiashara kuendelea kujiunga na kuwa na vigezo vinavyotakiwa vya ubora kwa ajili ya mradi wa bomba la mafuta, SGR Lot 3, na 4 pamoja na mradi wa Gas.

3.) Ushiriki katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini
TPSF inashirikiana na wanachama, wadau wa maendeleeo, na Serikali katika kupitia maboresho mbalimbali ili kuleta tija na mifumo rafiki ya ufanyaji wa biashara nchini. Mafanikio yaliyopatikana ni utekelezaji wa mpango kazi wa maboresho ya ufanyaji wa biashara nchini yaani (Blueprint for Regulatory Reform). Jumla ya maboresho 233 mbalimbali yamefanyika na kazi inaendelea.

TPSF pia ilishiriki kikamilifu katika mazungumzo ya kuondoa vikwazo vya biashara ambavyo si vya kodi (Non-Tariff Barriers) kati ya Tanzania na Kenya. Juhudi hizi zilipekea ripoti ya vikwazo hivyo kupelekwa kwenye Kamati ya Taifa ya Kuratibu vikwazo hivyo na kufanyiwa kazi. Tunayo furaha kuona kwamba zaidi ya vikwazo 40 (kati ya takribani vikwazo 60) vimeondolewa.

4.) Ushiriki katika Kufanikisha Mkutano wa 12 wa Baraza la Biashara
TPSF kwa kushirikiana na TNBC tulifanikisha uandaaji wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara uliofanyika tarehe 26 Juni 2021, Ikulu, Dar es Salaam.

Mkutano ulitoa maazimio saba (7) ambayo Mwenyekiti wa Baraza la Biashara Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan aliiagiza Serikali na Sekta Bifasi kuyatekeleza kabla ya Mkutano wa 13 wa TNBC, unaotarajiwa kufanyika Disemba mwaka huu. Sambamba na malengo mengine,Maazimio hayo yana lengo la kuboresha mazingira ya biashara na kukuza uwekezaji Tanzania.

Sekta binafsi inaendelea kushirikiana na TNBC kwa karibu na kufuatiliza utekelezaji wa makubalianao ya mkutano wa 12 wa Baraza la Taifa la Biashara.

5.) Ushiriki katika mchakato wa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/2021
TPSF imeshiriki mchakato wa maandalizi na mapokeo ya bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2020/2021 kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango. Hii ni pamoja na; kukusanya na kupeleka mapendekezo ya kikodi ya sekta binafsi; kushiriki katika midahalo na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kikosi kazi cha maboresho ya sera kikodi (Tax-Force on Tax Reforms); kushiriki katika vikao vya kamati ya bunge ya bajeti; na pia kuwemo katika Timu Maalum ya Wataalam ya Kumshauri Waziri wa Fedha na Mipango (Think Tank), kuhusu nini kiingie kwenye muswada wa bajeti 2020/2021.

Ndani ya huu mchakato tulifanikiwa kuwasilisha mapendekezo mengi yaa kisekta yakiwemo kupunguza ama kufuta tozo, ushuru na kodi mbalimbali. Mh.Mgeni Rasmi,asilimia kubwa ya mapendekezo ya sekta binafsi yalikubarika na kuingizwa kwenye sheria ya fedha ya mwaka 2020/21.

6.) Mikutano na Makongamano ya Biashara
TPSF imeshiriki ziara na mikutano ya kibiashara nchini Kenya, Burundi mikutano hii tulishiriki kuiandaa kwa kushirikiana na Wizara ya mambo ya nje, Wizara ya biashara na Viwanda kupitia TANTRADE,Mikutano hii imesaidia kuondoa baadhi ya vikwazo visivyo vya kikodi na pia kujenga uhusiano mzuri kati ya wafanyabisahara wa Tanzania na nchi hizi.

Mheshimiwa Mgeni rasmi: Tunakushukuru wewe binafsi kwa miongozo na ushauri ambayo umeendelea kutupatia katika eneo hili la Kuandaa makongamano. Tarehe 20-07-2021 Ulipotuita kwenye kikao cha wadau wa bandari ulitushauri Sekta Binafsi tuandae makongamano makubwa ya ndani na nje ya nchi na ukatueleza utayari wa viongozi wa serikali kushiriki makongamano ambayo sekta binafsi itayaandaa ndani na nje ya nchi. Napenda kukujulisha kuwa kazi hiyo tumeianzakwa kuandaa kongamano la sekta binafsi ya Tanzania na Sekta Binafsi ya Marekani ambalo lilifanyika mwezi September nchini Marekani na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, vile vile tumeweza kuandaa kongamano la pamoja na Sekta binafsi ya Uganda la Bomba la Mafuta. Kongamano hilo lilihudhuriwa na Marais Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Rais Kaguta Yoweri Mseveni Rais wa Jamhuri ya Uganda.

Sekta binafsi tumeshirikiana na Wizara ya Utalii kwenye Maonesho ya Utalii ya Africa Mashariki yaliyofanyika Arusha. Tunampongeza Waziri wetu Dr. Damas Ndumbarokwa jitihada zake za kuleta maonesho haya nchini kwetu na kufanyika kwa mara ya kwanza.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi hata Kongamano hili la leo ni matokeo ya mwongozo na ushauri ambao uliutoa kwetu.

Mheshimiwa mgeni Rasmi Naomba pia nichukue fursa hii kukushukuru kwa kazi kubwa ambayo umeifanya kuwezesha upatikanaji masoko makubwa ya bidhaa za kilimo. Ulipokuwa Mgeni Rasmi kwenye Kongamano la uwekezaji la bidhaa za mboga mboga lililoandaliwa na TAHA tuliiomba serikali isaidie kufungua soko la parachichi kwenye nchi ya Africa ya Kusini pamoja na India na ulitoa maelekezo palepale kwa Wizara ya kilimo kulifanyia kazi swala hilo kwa haraka. Tayari tumepokea taarifa kutoka Wizara ya Kilimo kuhusu kusainiwa makubaliano ya uingizaji wa zao la parachichi kwenye nchi za Africa Kusini na India.

 1. Eneo la saba ambalo tumefanikiwa ni kutengeneza Directory kwa ajili ya kampuni za Tanzania: Tayari tumeingia makubaliano ya kutengeneza directory yetu ya sekta binafsi ambapo kampuni zitajisajili, directory hii pamoja na mambo mengine itakuwa na taarifa muhimu za kampuni zikiwemo kiwango cha uwekezaji, mipango ya upanuzi wa biashara, idadi ya wafanyakazi, sekta, certification mbalimbali za ndani na za kimataifa n.k Directory hiyo itasambazwa katika balozi zetu kwenye nchi mbalimbali na baadae itakuwa kwenye mtandao ili mwekezaji anapotafuta mbia iwe rahisi kupata taarifa zake na hata urahisi wa kujua huduma zitolewazo na kampuni husika.
 2. Eneo la 8: Mapitio ya Sera, Kanuni na Sheria
  TPSF imeshiriki kupitia sera na sheria mbalimbali zenye lengo la kuimarisha mazingira ya biashara nchini na kuvutia uwekezaja kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, zikiwemo: Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini; Kanuni za Fedha za Kigeni, Sera ya Biashara, Sera ya Manedelea ya Viwanda, Kanuni za Sera za Viwanda n.k.
 3. Eneo la Tisa: Africa Franchising Accelerator Project (AFRAP)
  TPSF inatakeleza mradi wa AFRAP kutoka kwa Benki ya Maendeleo Africa (AfDB). Mradi huu una lengo kuu la kukuza na kutoa mfano wa mkakati wa kitaifa wenye nguvu wa maendeleo ya biashara barani Africa, kwa kuzingatia maeneo huru ya biashara ya bara la Africa (AfCFTA). Kwa kutumia Tanzania kama majaribio, ufadhili unatarajiwa kuleta ushirikiano wa kiuchumi wa haraka zaidi, kidiplomasia ya kibiashara, uhusiano wa haraka wa ujuzi, uundaji wa nafasi ya kazi, uzalishaji mali na kupunguza umaskini barani Africa.
  a) Malengo ya mradi huu ni:
  b) Kusaidia na kulea kampuni ndogo na za kati (SMEs) 90 za kiasili na mabadiliko 10 ya waendeshaji wadodo wadogo kuwa chapa za biashara
  c) Kuiunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuandaa sera ya ukodishaji na kuunganisha ubia katika sera nyingine zinazohusiana na biashara
  d) Kuanzisha Franching Asssociation of Tanzania (FATA) ili kiwe chombo cha udhibiti wa sekta wakati wa kufunga mradi

Eneo la 10: Ushirikiano naTradeMark East Africa (TMEA) kwenye majukwaa ya Mazungumzo ya Sekta binafsi na Sekta ya Umma
TPSF imeendelea kutekeleza mradi wa TMEA wenye lengo la kuendeleza midahalo kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPD) wenye lengo la kukuza biashara na uwekezaji nchini Tanzania. Mradi huu umekuwa chachu ya mabadiliko ya mazingira ya biashara.Umewezesha kupitia sera, kanuni, sheria na taratibu, midahalo kati ya sekta binafsi na sekta ya umma inayohusiana na uwekezaji na biashara, utafiti, maswala ya kodi na mazingira ya biashara kwa ujumla. Hii imetoa na inaendelea kutoa nafasi kwa sekta binafsi kushiriki shuguli muhimu za nchi na midahalo mbali mbali ya ndani na nje ya Tanzania yaani majukwaa ya biashara ya ndani ya nchi na kikanda na nchi

Eneo la 11:Ujuzi wa Ubunifu (Creative Skills) – UNESCO
TPSF inatekeleza mradi wa Ujuzi wa Ubunifu kwa ufadhili wa UNESCO. Mradi unalenga kusaidia unanzishwaji wa Baraza la Ujuzi la Sekta ya Ubunifu katika Ngazi ya Taifa wenye lengo la kuwakilisha sekta hii na kuchochea ukuwaji wa sekta. Hii imetoa nafasi kwa wadau wa sekta ya ujuzi na ubunifu kukutana na kujadili vipaumbele vya sekta, pamoja namikakati itakayowasaidia. Pia kupitia mradi huu, TPSF inaandaa mpango mkakati wa miaka mitano wa baraza la ujuzi wa ubunifu.

 1. CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA KWA WANACHAMA MWAKA2020/2021
  Ugonjwa wa UVIKO-19
  Mheshimiwa Waziri Mkuu,ni takriban miezi 22 (16 Machi 2020) tangu Tanzania iliporipoti kesi yake ya kwanza ya UVIKO-19. Tumeshuhudia uchumi za nchi nyingi duniani zikidorora na nchi zikipoteza nguvu kazi, huku jamii zikiendelea kupoteza wapendwa wao. Hapa kwetu, kwa upande wa shughuli za kiuchumi, athari kubwa imeonekana kwenye sekta za kiuchumi kama vile Utalii na zile zingine ambazo utegemea soko la nje na malighafi kutoka nje kama Sekta ya Viwanda.

Ata hivyo, janga hili pia limezua mageuzi makubwa ya ufanyaji biashara na tumeshuhudia teknolojia ikichukua nafasi kubwa katika kuwezesha msingi wa mabadiliko haya.

Katika kipindi hiki, wafanyabiashara wa Tanzania pia wameonyesha utofauti, uwepesi (flexibility) na ustahimilivu (resilience) wao wa kukabiliana na majanga kwa kuunda mifumo mipya ya biashara (business Models).

UVIKO-19 ni changamoto na fursa hasa kwenye mazao ya kilimo ya kikanda. Kenya, Uganda, Rwanda na nchi za SADC.

Mhe. Mgeni Rasmi, Sekta Binafsi ya Tanzania isingeweza kufika hapa bila sera, mikakati na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya sita ikiwepo kuwezesha upatikanaji wa chanjo bure kwa wote pamoja ikiwemo kuiwezesha sekta binafsi kunufaika na TZS 1.3 trilioni iliyopokelewa hivi punde na serikali kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ili kujenga uwezo wa ndani wa kukabiliana na athari za janga ili la UVIKO-19.Katika hili, nichukue nafasi hii kuhimiza Sekta Binafsi kutimiza majukumu yake kwa kuzingatia weledi na uadilifu wa hali ya juu, ili kuenzi imani ya serikali kwetu.

 1. MIPANGO YETU YA MBELE 2021/2022
  Mweshimiwa Waziri Mkuu,
  i. Taasisi yetu imeanza hatua za awali za kupitia mpango mkakati wetu wa miaka mitano, ili kuhakikisha kwamba inashabiiana na maendeleo mapya ya kiuchumi na matarajio ya nchi yetu, kama vile mpango wa mendeleo wa miaka mitano wa awamu ya tatu (FYDPIII). Hili litatekelezwa sambamba na mapitio/marejeo ya katiba yetu ya Taasisiyenye lengo la kuiboresha zaidi.Tunaamini haya yote yatakamilika mwishoni mwa robo ya kwanza ya mwaka ujao (2022).

ii. TPSF itaendelea kushirikiana na wadau wa Sekta Binafsi pamoja na Serikali, katika kujadili sera mbalimbali, uboreshaji wa biashara na kuondoa kero zinazokwaza ufanyaji mzuri wa biashara nchini.
iii. Tutaendelea kuhimiza wadau wa sekta binafsi kushiriki katika majukwaa, makongamano, maonesho mbalimbali ya biashara ya ndani na nje ya nchi ili kujifunza, kutengeneza urafiki na kuvutia wawekezaji kuja nchini kwetu.
iv. Tutaendelea kuwajengea uwezo wanachama katika eneo la mafunzo ya kufanya utafiti na kuandika mapendekezo ya kisera, kikodi na kuboresha mazingira ya kibiashara (Tax, Policy & Business Environment Proposals).

v. Tutaendelea kutoa elimu kwa wadau wa Sekta Binafsi kuhusu soko huru la Afrika (AfCFTA), ili wadau wapate kujiandaa kwa kujua taratibu za kufuata na kushiriki katika fursa zipatikanazo na soko hili.

vi. TPSF inashirikiana na UNIDO kwenye mradi wa maeneo tengefu ya biashara - yaani “Industrial Parks” kwa kushirikiana na wadau wengine kama TAFOPA Mradi huu unaitwa Tanganyika Packers Special Agro industrial Processing Zone (TP-SAPZ), Lake Zone, Tanzania. Naomba kuchukua nafasi kumshukuru Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kulipa kipaumbele swala la ujenzi wa maeneo Tengefu pamoja na juhudi zake za kutafuta fedha za wafanyabiashara ndogo ndogo na akina mama kutoka Benki ya Maendeleo ya Africa.

vii. Tutaendelea kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, kuleta miradi inayochagiza maendeleo ya biashara, hasa kilimo-biashara na kuongeza thamani ya mazao, utalii, utafiti wa data za biashara na program ya vijana na wanawake walio katika biashara.

viii. Pia itaendelea kukuza stadi za kazi na progamu mbalimbali za mafunzo. Tutashirikiana na wadau waliokwishaonesha nia kama Benki ya Dunia, Ubalozi wa Canada, Ubalozi wa Ujerumani kupitia GIZ, Ubalozi wa Marekani kupitia USAID, Umoja wa Ulaya na Ubalozi wa Uingereza kupitia UKAid na wadau wengine

Mhe. Mgeni rasmi,

Katika kutimiza lengo la kuwa moja ya taasisi kuu (Apex organizations) za sekta binafsi zenye ushawishi mkubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bodi na sekretarieti ya taasisi imejitolea kufanya yafuatayo

i. Katika kuhakikisha tunaongeza ushawishi wetu katika mapendekezo au mabadiliko ya kisera, sheria n.k, taasisi yetu imejipanga kuwekeza zaidi kwenye deta (data) na takwimu (empirical analysis). "Simply envsioning to have Big Data." Haya yote tutayafanikisha kwa ushirikiano na taasisi za utafiti ndani na nje ya nchi, na pia kupitia wadau wetu wa maendeleo.

ii. Vilevile, tunaahidi kuhimiza ufanyaji biashara ulio wazi na shindani lakini pia ulipaji wa kodi sahihi na stahiki kwa serikali yetu. Lengo ni kuenzi kiwango cha imani ambayo serikali yetu imeendelea kuipa Sekta Binafsi kupitia taasisi yetu. "Kwenye hili tutakuwa waaminifu sana."

iii. Tumejipanga kufanya kazi kwa karibu na taasisi nyingine za sekta Binafsi za kitaifa, kikanda na kimataifa ili kuhakikisha tunaunda umoja (alliances) ambao utawezesha ufanyaji biashara ya kikanda, kuruhusu uwekezaji na kurahisisha uhamisho wa ujuzi (transfer of skills and knbowledge).

iv. Mwisho, Taasisi yetu itaendelea kubainisha na kukamatia fursa katika miradi ya kimkakatiinayoletwa na wadau wetu wa maendeleo yenye tija kwa wanachama wetu lakini pia kwa manufaa ya kuboresha ufanyaji biashara na uwekezaji ili kuimarisha uchumi wetu.

 1. MAOMBI YETU KWA SERIKALI YA JMT

Mheshimiwa Waziri Mkuu,
Ulivyokutana na viongozi wa TPSF tarehe 27 Januari mwaka huu, kuna baadhi ya changamoto za Sekta Binafsi tuliziwakilisha kwako. Tunapenda kuishukuru serikali kwa kutatua idadi kubwa ya hizi changamoto katika kipindi kifupi.

Mheshimiwa Waziri Mkuu,
Pamoja na mafanikio haya, ninaomba uniruhusu nikutaarifu baadhi ya changamoto nyingine ambazo ni muhimu zitatuliwe ili Sekta binafsi iweze kuchangia kikamilifu katika uchumi wetu:

(a) Kutokuwepo kwa Sera rasmi na Mkakati wa Maendeleo ya Sekta Binafsi (Private Sector Development Policy and Strategy). Mh. Waziri Mkuu, bado sekta binafsi inaendelea kuwasilisha ombi kwa serikali la kuiwezesha iweze kutoa mchango mkubwa zaidi kwenye uchumi wetu lakini pia kujidhibiti na kuviwezesha vyama vya biashara vya kisekta (sector specific PSOs) kuendesha shughuli zake
(b) Kutungwa kwa Sera ya kuwezesha wananchi na makampuni ya Kitanzania (Local content Policy): Mh. Waziri Mkuu, utakumbuka, suala hili tulilizungumzia katika kikao cha 12 cha Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) kilichofanyika mwezi Juni mwaka huu. Tunaipongeza serikali, kupitia Ofisi yako kwa juhudi zilizoanza za kuja na sera hii. Hivyo basi, tunaendelea kuishauri serikali iharakishe zoezi hili kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha sera hii inaweza kutatua changamoto zilizopo na kuhainisha fursa mbalimbali.

(c) Kuwekeza katika Ujuzi (Skills)-Kuna Gap kubwa sana la elimu inayotolewa na kinachohitajika kwenye soko. Vyuo vifanye kazi na Sekta binafsi kujua nini kinahitajika kwenye soko. Kazi za managers kwenye viwanda ni chache tunahitaji mafundi.

(d) Interest rate-Ipo juu kampuni za kitanzania ni masikini na haziwezi kukua zinapata mikopo bank watu wanapata utajiri bandia wa muda mfupi akianza kulipa marejesho ya bank anafilisika. Interest rate ya asilimia 20 huwezi kutengeneza utajiri na huwezi kushindana na kampuni inayotoka nje na mkopo wa 2 percent ukashindana nayo. Matajiri wengi hata Watanzania mikopo yao mingi mikubwa wanaipata nje na wengine walipata bahati ya kupata Government Guarantee hapo nyuma. Tunamshukuru Mh. Rais kwa kuyaagiza mabenk kushusha interest. Zipo ambazo zimeanza kushusha kwenye sekta ya kilimo. Tunaomba pia sekta ya utalii isaidiwe.

(e) Ushirikishwaji wa Sekta binafsi kwenye mikataba ya uwekezaji wa kimkakati kabla na katikati ya mazungumzo ili sekta binafsi iweze kujiandaa katika ushiriki kwa kujua mahitaji ya mradi na vigezo vinavyohitajika.

(f) Changamoto kwenye Self regulating (Sekta binafsi inayojisimamia yenyewe) sekta binafsi ni pana ni Zaidi ya asilimia 95 ya Watanzania wote- bila structure ambayo inasimamiwa na sheria, taratibu na kanuni sekta binafsi haiwezi kujisimamia yenyewe- Tunaomba Serikali Wizara ya uwekezaji sera ya Sekta binafsi ambayo tumeiomba muda mrefu. Wawekezaji wanakuja wanaliza na serikali wanaanza kazi kesho wakiharibu utasikia sekta binafsi haifai wakati hao wasiofaa hata hatuwafahamu. Leo tuna wizara inayoshughulika na Sekta binafsi lakini nikiwa na tatizo linalohusu maliasili nitaambiwa niende maliasili, nina magari yamekwama na magogo DRC nitaambiwa nenda wizara ya mambo ya nje au viwanda na biashara. Ni Muhimu vitu vikawa structured vikaeleweka.

(g) Serikali iwezeshe kampuni za kitanzania kwenye maeneo ambayo ni strategic ili kampuni hizi ziweze kutoka nje kwenda kushindana. Tumeingia kwenye ACFTA hatutaweza kushindana kama hatuna kampuni strong za kuweza kushindana. Makampuni mengi yanayotoka nje kuja kuwekeza mengi yanakuwa na nguvu ya serikali zao nyuma. Kunatakiwa kuwe na deliberate move ya serikali kuziwezesha kampuni za ndani.
(h) Miradi ya Public-Private Partnerships (PPP): Tunaipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, kwa kuendelea kuainisha miradi mbalimbali ya ubia kwenye Mipango ya maendeleo ya kila mwaka na kuipa kipaumbelesekta binafsi ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi hiyo. Hata hivyo, ili kuongeza tija na ufanisi, tunashauri TPSF ishirikishwe kuanzia hatua za uhibuaji na uandaaji wa mikakati ya kutangaza fursa zitakazojitokeza, ili kuwezesha sekta binafsi ishiriki kikamilifu.
(i) Kuwekeza kwenye utafiti (Research & Development): Tunaendelea kushauri vitengo vya utafiti kwenye kila wizara za uzalishaji vitengewe bajeti ya kutosha,na vitengo hivyo vihimizwe kushirikiana na taasisi na makampuni binafsi kwenye kufanya tafiti mbalimbali, zenye kutatua changamoto na kuibua fursa za kufanya biashara na uwekezaji ndani na nje ya nchi.

(j) Mikopo ya makampuni ya Utalii kwenye mabenki mbalimbali yaliyoathirika na UviKo 19

(k) Madeni ya watoa huduma: Malipo kwa watoa huduma hasa kwenye Halmashauri mbalimbali inarudisha nyuma juhudi za sekta binafsi. Watu waliotoa huduma kwenye halmashauri ni wafanyabiashara wadogo wadogo Watanzania. Hawawezi tena kukopesheka na mabenki na wengi wamefilisika. Kuna madeni ya miaka mitatu mpaka mitano kwenye halmashauri na kuna mtindo umezuka kwa wakurugenzi kusema deni hili sio la wakati wangu. Mheshimiwa Waziri mkuu tunaomba uingilie kati swala hili hali ni mbaya.

 1. HITIMISHO
  Mheshimwa Waziri Mkuu
  Naitimisha kwa kukushukuru tena kwa kutoa muda wako kuja kutufungilia Mkutano wetu Mkuu wa 21, na kuongea na wadau na wanachama wetu wa Sekta Binafsi na wenye mapenzi mema na maendeleo ya biashara nchini. Nakuomba twendelee kushirikiana kwa ukaribu ili Sekta Binafsi iendelee kuwa injini ya uchumi Tanzania kama wote tunavyo tamani. Mwisho kabisa naomba nichukue nafasi hii kukutakia wewe na wadau woteheri ya mwaka mpya.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

MUNGU IBARIKI SEKTA BINAFSI
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRIKA