JUKWAA LA 12 LA UNUNUZI WA UMMA KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

PPRA, kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha na Mipango, PPAA, GPSA na PSPTB, inapenda kuwakaribisha wadau wa ununuzi wa umma kwenye Jukwaa la Ununuzi wa Umma kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki litakalofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 29 Novemba, 2019. Jukwaa hili litafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC – Jijini Arusha.

Kaulimbiu  ya Jukwaa hili ni, “Matumizi ya Njia za Kisasa katika Ununuzi wa Umma kwa Maendeleo Endelevu ya Kiuchumi.”

Watakaohudhuria ni wadau wa ununuzi wa umma nchini, wakiwemo maafisa masuuli, wataalamu wa ununuzi kutoka taasisi za umma na binafsi, wajumbe wa bodi za zabuni, wakaguzi wa ndani, na wawakilishi wa idara tumizi. Vilevile, Jukwaa hili litahudhuriwa na watoa huduma serikalini, wazabuni, wafanyabiashara, wakandarasi na wanazuoni.

Sambamba na tukio hili, kutakuwepo na maonesho maalum ambapo taasisi za umma na binafsi zitapata fursa ya kutangaza huduma na bidhaa zao kwa washiriki wanaotarajiwa kuwa zaidi ya 400. Tafadhali, unaombwa kuthibitisha ushiriki wako kwa kulipia kiasi cha TZS. 350,000/= (Laki Tatu na Elfu Hamsini) tu; kwa kila mshiriki kabla ya tarehe 15 Novemba, 2019.

Kwa mawasiliano zaidi ya namna ya kushiriki Jukwaa au Maonesho, tafadhali wasiliana nasi kwa simu  namba +255 715 23 27 12 au baruapepe: eapf@ppra.go.tz 

Nyote Mnakaribishwa