Ndugu Wadau wa Sekta Binafsi,
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa kushirikiana na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) inakukaribisha kutoa maoni na mapendekezo kuhusu marekebisho ya sheria ya haki miliki namba 7/1999 Kama ilivyorekebishwa mara kwa mara.
Kufuatia marekebisho ya Sheria ya Fedha namba 5 ya mwaka 2022 Serikali ilifanya marekebisho katika Sheria ya Hakimiliki kwa kuanzisha tozo ya kulinda hakimiliki ifahamikayo kama “blank tape levy/blank tape remuneration” ya 1.5% kwenye vifaa vinavyotumika kuzalisha, kusambaza, kudurufu na kutunza kazi za Sanaa, uandishi na ubunifu.
Katika marekesho hayo sheria ilitaja vifaa vya aina sita kuanza kutozwa tozo pindi vinapoingizwa ama kutengenezwa hapa nchini. Moja ya vifaa hivyo ni vinasa sauti na CD/DVD.
Hivyobasi unakaribishwa kuhudhuria kikao hiki ili kutoa maoni na mapendekezo ya kuongeze vifaa.
Kupata nakala ya Andiko la Muswada huo kutoka COSOTA tembelea link ifuatayo:
WASILISHO KUHUSU UTEKELEZAJI NA MAPENDEKEZO YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA FEDHA Na.5 YA MWAKA 2022 SEHEMU YA VII, KIFUNGU CHA 27 (KIFUNGU CHA 48A(1)) KILICHOREKEBISHA SHERIA HAKIMILIKI NA HAKISHIRIKI (SURA YA 218) KUHUSU PRIVATE COPYING /BLANK TAPE LEVY OR REMUNERATION
Kikao hiki kitafanyika:
🗓️Tarehe: March 1,2023.
🕒Saa tisa kamili alasiri
📍Ofisi za TPSF zilizopo Masaki Mwaya Road, Dar Ess Salaam
Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na Ms. Jackline Isaack kupitia namba +255 717 577 217 au barua pepe jackline.isaack@tpsf.or.tz
TPSF Secretarieti .