TPSF NA CHANNEL 10 KUIMARISHA USHIRIKIANO KATI YAO ILI KUKUZA UWEKEZAJI NA USHIRIKI WA SEKTA BINAFSI KATIKA KUKUZA UCHUMI TANZANIA

Mkurugenzi wa Sera, Uraghibishaji na Huduma kwa Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Ndg. Zachy Mbenna wiki hii alimtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Africa Media Group Limited (AMGL) Bw. Shaaban Kissu na kujadili namna ya kukuza USHIRIKIANO baina ya Taasisi Hizi MUHIMU, AMCL na TPSF ili kuamsha na kuchochea ari vya uwekezaji nchini Tanzania, hasa kwa wazawa na makundi Maalum kama Wanawake, Vijana na Wasomi. Pia kutoa habari chanya na muhimu zinazohusu Sekta Binafsi na Uchumi wa nchi.

Akizungumza katika kikao hicho Bw. Mbenna alikipongeza chombo cha Habari cha AMGL chenye vituo mbalimbali ikiwemo kituo cha luninga cha Channel 10 kwa kufanya kazi kwa weledi na kusimamia misingi ya uandishi wa Habari. Pia aliutambua mchango wao katika kutangaza kazi zinazo fanywa na Sekta Binafsi Tanzania na jitihada za Serikali katika kuweka Mazingira Bora ya Biashara na Uwekezaji. Pamoja na pongezi, Ndg. Mbenna aliwaomba AMCL kuendelea kuunga mkono shughuli na jitihada zinazofanywa Sekta Binafsi katika kujenga Uchumi na kuleta Maendeleo nchini.

Kwenye kikao hiki muhimu Bw Mbenna na Bw. Kissu walikubaliana kushirikiana kuandaa vipindi vitakavyoibua ari ya uwekezaji na uzalishaji mali kwa makundi ya Vijana, Wanawake na Wasomi. Wakurugenzi hao pia wamekubaliana kila upande kutoa rasilimali zake ili kutangaza shughuli za Sekta Binafsi na Manufaa yake kwa nchi na jamii kwa ujumla.