TPSF YAKUTANISHA WADAU WA SEKTA BINAFSI ILI KUPOKEA MAONI KUHUSU MUSWADA MPYA WA SHERIA YA UWEKEZAJI.

Tarehe 18 Oktoba, 2022; Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imefanya kikao cha kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi nchini ili kuupitia muswada mpya sheria ya uwekezaji kwa lengo la kupokea maoni na mapendekezo yao. Maoni haya yatapelekwa kwenye kamati ya bunge inayo shughulikia maswala ya sheria pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

Wadau wa sekta binafsi walioshiriki kikao hiki kutoka ukumbi wa Hoteli ya New Africa, Dar es Salaam

TPSF imefanya kikao hiki kuitikia wito wa Waziri wa Uwekezaji Dk. Ashatu Kijaji uliowataka Wadau wa Sekta Binafsi kutoa maoni yao juu ya muswada huu kabla ya kupitishwa bungeni.

Wadau walio shiriki mkutano huu waliipongeza serikali kwa kwakuwapa fursa ya kutoa maoni yao na kuomba maoni hayo ya pewe kipaumbele na kutekelezwa. Pia wanatarajia kwamba muswaada huu utatoa ufumbuzi wa changamoto nyingi zinazo ikabili Sekta binafsi hivyo kuhamasisha uwekezaji wa ndani na nje.

Mdau wa sekta binafsi akitoa hoja yake kwenye kikao hiki kilichoandaliwa na TPSF kwa udhamini wa TradeMark East Africa

Muswada huu mpya wa uwekezaji uliotoka Agosti 31,2020 ukipitishwa utachukua nafasi ya sheria ya uwekezaji iliyopo sasa ambayo ilipitiswa mwaka 1997.

Wadau wa Sekta Binafsi walioshirki kwenye kikao hiki kupitia njia ya mtandaoni

Kiao hichi kiliuzuliwa wadau kadhaa ikiwemo wadau wa sekta ya afya, kilimo, viwanda, tehama, huduma na sheria.